Mahakama Kuu ya Tanzania leo inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi ya kupinga kuenguliwa kwa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, hatua ambayo huenda ikaathiri mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu. Kesi hiyo imepewa kipaumbele kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa na ACT-Wazalendo, ikidai kuwa uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume […]