Serikali yaombwa kupunguza gharama upatikanaji vibali, usafirishaji bidhaa mipakani

SERIKALI imeombwa kupunguza gharama zilizowekwa kisheria za upatikanaji wa vibali pamoja na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hasa za kilimo, viwanda na madini katika maeneo ya mipakani. Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Shirika linalojihusisha na ufanyaji wa tafiti mbalimbali za biashara na uwekezaji la Liberty Spark, Evance Exaud wakati wa uzinduzi …