Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, imemuamuru Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, kuanza na kukamilisha uchunguzi wa malalamiko ya wizi yaliyowasilishwa ofisini kwake na Radhika Pankanj dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wake (Mukesh Menaria).