Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na uharibifu mkubwa wa misitu unaochochewa na biashara ya kuni na mkaa. Nishati hii, inayotumika kwa wingi katika kupikia, husafirishwa kutoka Kilosa kwenda kuuzwa kwenye miji na majiji mbalimbali nchini.