Jenerali Moses Ali anavyoutaka tena ubunge akiwa na miaka 86

Madaraka matamu, ndiyo unavyoweza kusema baada ya Naibu Waziri Mkuu wa Pili na Mbunge wa Jimbo la Adjumani Magharibi mwa nchi ya Uganda, Jenerali Moses Ali (86), kusisitiza kuwa bado anautaka ubunge ili atumikie wananchi.