Miundombinu ndiyo injini ya maendeleo na ukuaji wa uchumi wa taifa lolote. Nchi yenye barabara za kisasa, bandari bora, reli za kisasa na viwanja vya ndege vyenye viwango vya kimataifa pamoja na madaraja imara hujipatia fursa kubwa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.