Ujenzi barabara, madaraja ulivyofungua fursa za kiuchumi Tabora

Wananchi wa Wilaya za Igunga na Nzega mkoani Tabora sasa wamepata ahueni baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara na madaraja mapya yaliyo chini ya mradi wa Rise unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), hatua hiyo imewaondolea kero ya usafiri na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii zilizokuwa zikikwamishwa na miundombinu duni kwa miaka mingi.