Mahakama yamkuta na hatia mwana-Tiktok kwa kukejeli familia ya Rais Museveni

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu Entebbe nchini Uganda imemkuta na hatia mtumiaji wa Tiktok, Juma Musuuza, maarufu Madubarah, kwa makosa sita, yakiwemo kutoa maneno ya chuki na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Rais Yoweri Museveni, mwanae, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, na Spika wa Bunge Anita Among. Madubarah ambaye pia ni mfanyabiashara wa viatu alidaiwa kutumia akaunti yake ya TikTok kuposti video mwaka 2024 akimkejeli Rais Museveni na mwanawe, akisema “Ikiwa Museveni atakabidhi madaraka kwa mwanawe mlevi, nchi itaangamizwa ndani ya siku mbili.” Pia alimtuhumu Spika Among kwa kutumia vibaya fedha za walipa kodi kujenga jumba la kifahari kuliko Ikulu na […] The post Mahakama yamkuta na hatia mwana-Tiktok kwa kukejeli familia ya Rais Museveni appeared first on SwahiliTimes .