Wafanyabiashara wa chakula, vinywaji baridi, nyama choma, na vitafunwa katika viwanja vya Tanganyika Packers wameeleza kufurahishwa na mauzo mazuri kufuatia umati mkubwa wa watu uliokusanyika kushuhudia uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.