Walalamikaji katika kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameibua shauri dogo jipya, wakiiomba Mahakama iwaamuru walalamikiwa wawapatie nyaraka za chama hicho ili wazitumie kama ushahidi kuthibitisha madai yao.