Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma imeipa serikali siku tano kujibu madai yaliyotolewa Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina juu ya ukiukwaji wa katiba na kanuni za uchaguzi wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea wa urais. Hata hivyo, Ombi la upande wa Serikali la kuongezewa siku 14 kwa ajili ya kuwasilisha majibu limekataliwa. Aidha, mahakama hiyo imetamka kuwa licha ya zoezi la uteuzi kumalizika, endapo itajiridhisha kuwa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilikiuka katiba na kanuni kumzuia Mpina kurejesha fomu, haitasita kutoa amri ya kumpa fursa ya kurejesha fomu na kuteuliwa kugombea Urais. Kesi hiyo imesikilizwa […] The post Serikali yapewa siku tano kujibu madai ya Mpina appeared first on SwahiliTimes .