Matatani tuhuma kuisababishia TTCL hasara ya Sh1.5 bilioni

Mfanyabiashara na mkazi wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, Grey Chilaza na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kulisababishia hasara ya Sh1.5 bilioni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL ).