Yaliyojiri shauri la Mpina kugombea urais

Shauri la utata wa uteuzi wa mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 limetajwa mahakamani kwa mara ya kwanza, huku Mahakama ikisema haitasita kusimamia haki itakaporidhika kuhusu uwepo wa ukiukwaji wa taratibu.