Mamlaka nchini Kenya zimeanza uchunguzi dhidi ya raia wa Uhispania aliyenaswa kwenye video akimnywesha tembo bia katika hifadhi ya kibinafsi ya Ol Jogi Conservancy, Kaunti ya Laikipia. Video hiyo, iliyosambaa mitandaoni wiki hii, ilionesha mgeni huyo akimimina bia aina ya Tusker kwa tembo maarufu anayejulikana kwa jina la Bupa. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika […]