Samia aahidi lami, kituo cha afya Morogoro vijijini

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuboresha huduma za afya, barabara na kilimo kwa wananchi wa Morogoro vijijini endapo atachaguliwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.