Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewaonya wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwapeleka watoto kwenye vilabu vya usiku, likieleza kuwa maeneo hayo yanachochea mmomonyoko wa maadili na kuwaweka watoto katika hatari ya ukatili wa kijinsia na kiafya.