Aondolewa uvimbe wa kilo mbili kwenye pafu Hospitali ya KCMC

Jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) limefanikiwa kuondoa uvimbe mkubwa wenye uzito wa kilo mbili kwenye pafu la kushoto la kijana mwenye umri wa miaka 30, ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupumua kwa muda mrefu.