Katika kukuza kampuni changa nchini, Chama cha Kampuni Changa Tanzania (TSA) kimeingia makubaliano na kampuni ya uturuki ya AfrIcapital Investment Holdings Ltd, kwa lengo kusaidia na kuwezesha upatikanaji rahisi wa masoko na mitaji kwa biashara changa.