Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (CHADEMA), Gasper Temba, hajatekwa isipokuwa amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka. Taarifa hiyo imesema Temba amekamatwa kwa mujibu wa sheria, na taratibu nyingine za kisheria zinafuata. Aidha, Jeshi hilo limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki. The post Polisi: Tunamshikilia Mwenyekiti wa BAVICHA appeared first on SwahiliTimes .