Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa barabarani naendesha gari. Mara nikafika sehemu yenye barabara nyembamba. Mbele yangu upande wa kulia kuna gari inakuja, na upande wa kushoto kuna mkokoteni unakwenda ninapoelekea. Ikabidi nisimame kusubiri mwenye mkokoteni asogee mbele ili niweze kupita vizuri kwa usalama.