Mchakato wa uteuzi ulifanyika kwa ushirikiano kati ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), huku majina ya waliofaulu yakiwa tayari yamewekwa kwenye tovuti za taasisi hizo.