Mahakama yaamuru KKKT Konde kulipa Sh133.5 milioni michango ya wafanyakazi NSSF

Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mbeya imeiamuru Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Konde, kulipa michango ya wafanyakazi wake kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), zaidi ya Sh133.5 milioni.