Mpango wa Chaumma kikichukua dola Oktoba

Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimetangaza ajenda kuu zitakazotekelezwa iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza Tanzania, kikisisitiza nia yake ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Watanzania kupitia sera zinazolenga kuboresha maisha, kupambana na ufisadi na kuinua uchumi wa wananchi wa kawaida.