Wengine sita watiania ZEC urais wa Zanzibar

Harakati za kusaka Ikulu ya Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano ijayo zimeendelea kushika kasi, baada ya watiania kutoka vyama mbalimbali kujitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuwania nafasi ya urais kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.