Mgombea urais NLD alia na usawa, heshima

Wakati Chama cha National League for Democracy (NLD) kikiwa kimetangaza kuzindua kampeni zake Septemba 4, 2025 mkoani Tanga, mgombea urais wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo, ametoa tahadhari akidai kwamba kwa siku tatu tangu kuanza kwa kampeni, kuna viashiria vya kutokuwepo kwa usawa na heshima kwa wagombea urais.