Huduma ya mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) katika barabara ya Mbagala, ambayo awali ilitarajiwa kuanza leo Jumatatu Septemba mosi, 2025, imesogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa miundombinu muhimu yakiwamo mageti janja na kituo cha kujazia gesi.