Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo umefafanua kuhsu video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha muuguzi wa hospitali ya wilaya hiyo akitolewa kwa nguvu na mlinzi wa Suma JKT ndani ya wodi ya wajawazito, hali iliyosababisha sintofahamu miongoni mwa wananchi na wagonjwa waliokuwa wodini.