Serikali yatoa msamaha wa kutoshitakiwa kwa watakaosalimisha silaha haramu

Jeshi la Polisi limesema Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa msamaha wa kutoshitakiwa kwa wamiliki wa silaha kinyume cha sheria endapo watasalimisha silaha haramu kwa hiari kuanzia leo Septemba 01 hadi Oktoba 31, 2025. Taarifa hiyo imesema msamaha huo ni moja ya mikakati inayotekelezwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa mikataba, itifaki, maazimio na makubaliano mbalimbali ya kuzuia uzagaaji wa silaha ndogo na nyepesi. Wananchi wametakiwa kuwasilisha silaha hizo katika kituo chochote cha Polisi, ofisi ya Serikali za Mitaa au kwa Mtendaji Kata kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa […] The post Serikali yatoa msamaha wa kutoshitakiwa kwa watakaosalimisha silaha haramu appeared first on SwahiliTimes .