DODOMA : KATIKA mbio za kuwania kiti cha Rais na Makamu wa Rais kwa Uchaguzi Mkuu 2025, taifa linashuhudia rekodi ya kisiasa ikiandikwa baada ya wanawake watatu kujitokeza kuwania urais na 10 wakiwa katika nafasi ya makamu wa rais. Kujitokeza kwa wanawake watatu kuwania kiti cha rais kunavunja rekodi na kuweka idadi ya wanawake waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu kisiasa kufikia sita tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1995. The post Wanawake waandika rekodi mpya uchaguzi 2025 first appeared on HabariLeo .