Daraja jipya laibua kicheko kwa wasafiri, madereva

Wananchi, madereva na wasafirishaji waliokuwa wakikumbwa na changamoto kubwa ya usafiri kila msimu wa mvua eneo la bonde la maji, Ruvu, Kibaha mkoani Pwani, sasa wamefurahi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja jipya la mita tano lenye thamani ya Sh1.5 bilioni.