Baada ya huduma ya mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) katika barabara ya Mbagala kukwama kuanza leo kama ilivyoahidiwa awali na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), wachumi na wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa malalamiko pamoja na ushauri wa nini kifanyike ili huduma hiyo ianze kutekelezwa.