Salum Mwalimu aahidi Tanzania ya ‘maziwa na asali’

Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu amewaomba Watanzania kumchagua kwa kishindo ifikapo Jumatano Oktoba 29, 2025, ili alitengeze taifa lenye ustawi na neema, akiahidi kuigeuza Tanzania kuwa "nchi ya maziwa na asali' iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu.