Kero tano zinavyopigiwa chapuo na wagombea urais

Upatikanaji duni wa huduma ya maji safi na salama, migogoro ya ardhi, miundombinu, uhaba wa ajira na kipato kwa wananchi, ndizo changamoto zilizoteka vinywa vya wagombea urais wa vyama mbalimbali vya siasa ndani ya siku tano za mwanzo za kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.