Maarifa ya asili katika ukuzaji uchumi wa Taifa

Kila kizazi kina wazo, ndoto na azma yake ya kuweka alama mpya katika ukuaji wa taifa. Miaka mingi iliyopita, Tanzania ilijikita katika Dira 2025, iliyokuwa mwongozo wetu katika kujenga msingi wa uchumi wa kati. Leo, tunapaa mbali zaidi na kuzindua Dira mpya ya 2050.