Dkt. Samia Aahidi Uwanja wa Ndege Mpya Kagera, Kuchochea Utalii na Biashara

MISENYI, KAGERA — Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa katika eneo la Kyabajwa, wilayani Misenyi, mkoani Kagera, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo. […]