Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga umewasili katika uwanja wa ndege wa JKIA. Mwili huo unapokelewa na Rais William Ruto, aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, familia ya Raila Odinga na maofisa wengine wakuu serikalini. Ujumbe kutoka Kenya ulitumwa jana kwenda kuuchukua mwili huo nchini India ambako Raila Odinga alikuwa anapata matibabu. …