Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeyakataa maombi ya mawakili wa wajibu maombi katika shauri la kutekwa kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kuwaita kizimbani na kuwahoji watu waliokula viapo vilivyoambatanishwa katika hati ya maombi ya shauri hilo, akiwamo wakili wake, Peter Kibatala.