OMO aahidi mkakati kuinua sekta ya kilimo, wakulima

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema Serikali atakayoiunda itawajengea wakulima taaluma, kuwapatia mafunzo ya kisasa na kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ili waondokane na utegemezi na umaskini uliokithiri.