Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Miundombinu, Rogatus Mativila amewataka Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) kuzingatia kasi ya mabadiliko ya maendeleo ya dunia kwa kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora, usalama na uendelevu.