JWTZ lawaomba Watanzania kupuuza taarifa za uchochezi mitandaoni

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewaomba Watanzania kupuuza machapisho/ taarifa kwenye mitandao ya kijamii yenye lengo la kuleta uchochezi kwa kulihusisha Jeshi na siasa. Wananchi wamekumbushwa kuwa taarifa zote zinazolihusu Jeshi zitatolewa na Makao Makuu ya Jeshi kwa utaratibu rasmi. Aidha, Jeshi hilo limesema kuwa  linaridhishwa na hali ya usalama iliyopo nchini katika kipindi hiki ambacho vyama vya siasa vinafanya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, “Jeshi linaviomba vyama vya siasa kuendeleza hali ya amani, usalama na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi,” imeeleza taarifa […] The post JWTZ lawaomba Watanzania kupuuza taarifa za uchochezi mitandaoni appeared first on SwahiliTimes .