Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga jengo kubwa la kisasa la Machinga Complex mjini Bukoba, mkoani Kagera, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya serikali yake ya kuwainua kiuchumi wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga.