Vodacom yazindua Duka Mbagala ili kusogeza huduma kwa wateja wao

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc imezindua duka jipya la kisasa katika eneo la Mbagala Zakhem ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani. Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kampuni akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara, Bi Brigita Shirima, ambaye aliongoza zoezi la uzinduzi kwa kukata utepe, pamoja na Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Bi Happiness Shuma, na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Bi Belinda Wera. Pia walikuwepo washirika wa Vodacom wakiwemo wawakilishi kutoka kampuni ya Mayzon Group Limited wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Vishar Matambo. […] The post Vodacom yazindua Duka Mbagala ili kusogeza huduma kwa wateja wao appeared first on SwahiliTimes .