Benki Kuu yakanusha kuchapisha fedha kwa ajili ya uchaguzi

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa inachapisha na kusambaza fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu, huku zingine zikihamasisha wananchi kuondoa fedha zao kwenye benki kwa madai kuwa baadhi ya benki zimeishiwa fedha kutokana na uchaguzi. Taarifa ya Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel Tutuba, imeeleza kuwa BoT huchapisha fedha kwa mujibu wa Kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu, Sura ya 197, na kuziingiza kwenye mzunguko kulingana na shughuli za kiuchumi na mahitaji ya kubadilisha fedha chakavu, na siyo vinginevyo. “Napenda kuwathibitishia kuwa benki zote zilizopo nchini zinasimamiwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, […] The post Benki Kuu yakanusha kuchapisha fedha kwa ajili ya uchaguzi appeared first on SwahiliTimes .