Mshahara kima cha chini sekta binafsi waongezwa, waajiri watakaokaidi kukiona

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetangaza kima cha chini cha mshahara wa sekta binafsi ambapo sasa itakuwa ni ShSh358,322 kutoka Sh275,060 ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4.