BoT yakanusha kuchapisha fedha kugharamia uchaguzi

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa taasisi hiyo imechapisha fedha na kuzisambaza kwa ajili ya kugharamia uchaguzi mkuu, ikieleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote, ni upotoshaji unaolenga kupotosha umma.