SUA yapata miradi 36 yenye thamani Bil.10.5

CHUO  Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA ) kimeeleza kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu  miradi mipya ya utafiti 36 yenye thamani ya sh bilioni 10.5 imepatikana. Kati ya miradi hiyo 10 inafadhiliwa na wafadhili wa nje, miradi miwili ya Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na miradi 24 inafadhiliwa na Chuo Kikuu hicho kupitia mapato yake ya ndani. The post SUA yapata miradi 36 yenye thamani Bil.10.5 first appeared on HabariLeo .