Lema aitwa Polisi kuwasilisha madai yake

Jeshi la Polisi limemsisitiza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema kufika katika kituo cha Polisi ili awasilishe rasmi taarifa aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii juu usalama wake kuwa hatarini. Kupitia ukurasa wake wa X, Lema aliandika kuwa maisha yake yapo hatarini kutokana na kudai kuwa baadhi ya watu wanamfuatilia na hata kuonekana maeneo ya nyumbani kwake, hali inayomfanya kuwa na hofu juu ya usalama wake na familia yake. Aidha, Jeshi hilo limesisitiza baadhi ya viongozi na wananchi kuzingatia utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa sahihi kwa jamii na mamlaka za haki jinai ili kuepusha upotoshaji na taharuki zisizo […] The post Lema aitwa Polisi kuwasilisha madai yake appeared first on SwahiliTimes .