Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) imetangaza kima kipya cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi, ambacho sasa kitaanza kuwa Shilingi 358,322 kutoka Shilingi 275,060, ikiwa ni ongezeko la asilimia 33.4. Kima hicho kipya kitaanza kutumika rasmi Januari 1, 2026. Hatua hii inakuja miezi michache baada ya Serikali kupandisha kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1, kutoka Shilingi 370,000 hadi Shilingi 500,000, tangazo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, […] The post Serikali yapandisha kima cha chini cha mshahara Sekta Binafasi appeared first on SwahiliTimes .