SUA yalipa fidia ya Sh1.6 bilioni kwa wananchi kupisha upanuzi wa chuo

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimewalipa wananchi fidia yenye thamani ya zaidi ya Sh1.6 bilioni kufidia ardhi, mali na posho mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kifuta machozi kwa makaburi 18 yaliyokuwepo katika eneo lililotwaliwa kwa ajili ya upanuzi wa chuo.