Polisi wazungumzia madai ya Lema, kamatakamata Chadema

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikilaani wimbi la ukamataji, utekaji na vitisho vinavyoendelea dhidi ya viongozi na wanachama wake katika Kanda ya Victoria, hususani mkoani Kagera, Jeshi la Polisi limesema baadhi yao walikamatwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria kwa tuhuma za kihalifu.